Msanii wa kikundi cha Wasafi Rayvanny alizindua wimbo na video mpya ya ‘I love you’ kama majuma matatu yaliyopita na tayari imetazamwa zaidi ya mara milioni 2.5, katika mtandao wa Youtube.
Hata hivyo, video hiyo imezua tetesi tele katika mitandao ya kijamii huku mashabiki kadha wa kadha wakidai kuwa kuna puto au kondomu iliyotumika ambayo inaonekana kitandani. Kondomu hiyo inaonekana ikiwa imelaliwa na mwanadada kwa jina Nana.
Kwenye wimbo huo, Rayvanny anasema,
SURA YA MAMA, UMBO LAWAMA
NAYABIA MAGUU
UNANICHANGANYA UKIINAMA
NAANGALIA TATTOO
Kipande cha kanda hiyo ambacho kimezua maneno ni wakati ambapo Nana anaonesha michoro yake (Tattoo) na wakati kamera inaangazia michoro hiyo, mashabiki wanaona kitu kinachofanana na mpira wa kondomu kitandani.
Hata hivyo, mwandishi alipotazama video ile mara kadhaa alibaini kuwa haikuwa kondomu iliyotumika ila kilikuwa kipande cha ua, kinyume na jinsi wengi walivyodhania.
Tazama picha za kipande hicho cha ua,
Kulingana na blogu kadhaa kutoka Bongo, Nana na Rayvanny wanachumbiana na kuna tetesi kuwa huenda mrembo huyo ana mimba ya msanii huyo.
Rayvanny na mama ya mwanawe Fahyma walitengana juzi juzi na ilimbidi akimbie mtandao wa wa Insta kutangazia dunia kuwa hawako pamoja.
NIMEKUA NAKUHESHIMU MIAKA YOTE TULIOKUWA PAMOJA KUNA MENGI TUMEKOSEANA NA TUMESAMEHEANA NA MOST OF THE TIME UMEKUWA UKITAMANI MAISHA AMBAYO KILA SIKU NAKWAMBIA HAYATAKUSAIDIA …. NAKUHESHIMU NA NAISHEMU SANA FAMILIA YANGU …. IKIWA UMEAMUA MWENYEWE KUONDOA I WON’T BLAME YOU ….. STILL LOVE MY FAMILY …NAKUTAKIA MAISHA MEMA.
Fahyma naye alitumia fursa hiyo kumjibu kupitia mtandao huo huo na kusema,
HESABU MIMI NA JAY AMEFARIKI KWENYE MAISHA YAKO. I WILL FIGHT NA NITASHINDA. SITAKOSA PESA YA KULA. ILA MM NA JAY HESABU KUWA TUMEKUFA KWENYE MAISHA YAKO